Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei (kulia) akibadilishana mawazo na mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Msasani, mchungaji Elgard Metili wakati wa ibada maalum ya kumshukuru mungu kwa ajili ya mafanikio ya Benki ya CRDB katika kipindi cha mwaka 2014.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kushoto) akiwa na mke wake wakiwa katika ibada ya Shukrani kutokana na mafanikio waliyopata katika kipindi cha mwaka 2014.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakiwa katika ibada ya Shukrani.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Walitakiwa kwenda kwa wananchi kuwashukuru na sio kwenda kanisani tena katoliki sababu ni kwamba kimaadili wao wanahudumia watu wa dini mbalimbali na itikadi mbalimbali sasa atuambie kuwa wakurugenzi wote na mameneja ni wakatoliki? Na kama ni hivyo equality iko wapi hapo? Au ni bank ya kichaga kama inavyosemekana?

    ReplyDelete
  2. Nimesikitishwa sana na huu udini wa CRDB,iweje kama kushukuru kwa mafanikio ya kampuni au shirika yawe ktk kanisa ambalo labda mkurungenzi ndio anasalia?hii kweli inakuaja akilini?kwani wafanyakazi wote na wateja wa CRDB ni wahumini wa KKKT?kilichopaswa kufanyika ni tafrija ndogo yenye kujumuisha mchanganyiko wa salana dua,sio watu wote wafike KKKT kisa Big Boss ndio ana sali...shame on you CRDB...punguzeni udini...na kuwa wazalendo kwa kuwa fair....ankal ukibana hii comments najua una yako...ila wakifunze kuwa fair kwa wateja na wafanyakazi wengine.

    ReplyDelete
  3. e bwana hii ni kweli?
    kwani hii benki si ya wananchi?
    au ya dhehebu la kidini?
    sisi nasi tusio wakristo na ni wateja inakuwaje?
    maana kama ni benki ya dhehebu fulani tuelezwe wazi ili tujipange vizuri.
    nijuavyo taasisi zote zihusishazo wananchi wa aina tofauti basi inapobidi kufanywa maombi hushirikisha madhehebu zaidi ya moja, haya kwangu ni mapya kuona mambo yameishia kanisani tu. viongozi CRDB tufafanulieni nasi wateja wenu.
    shukran
    mteja akaunti ya TANZANITE
    Mndengereko ukerewe

    ReplyDelete
  4. Mimi nawaunga mkono sana CRDB, hongera sana Dr. Charles Kimei, bodi ya Wakurugenzi, Uongozi na Wafanyakazi wote, hapo mmemuheshimu sana MUNGU, naye atawaheshimu na kuwabariki. 2015 ni mwaka wenu. Ni lazima tufike mahali tutenganishe uwezo wetu kama wanadamu na uwezo wa MUNGU. Hata taifa la Marekani lilianzishwa kwa msingi wa YESU kristo, ndio maana lilikuwa taifa kubwa sana na lenye nguvu. Hata hela yao bado inamheshimu MUNGU ( IN GOD WE TRUST), ndio maana mpaka leo bado ina nguvu dunia nzima. MUNGU awabariki sana CRDB.

    ReplyDelete
  5. msilalamike tu hapa wapigieni tuendelee kuwaonyesha jinsi suala hili lilivotukera. Pigeni kwa namba yao ya huduma kwa wateja 0714197700.

    ReplyDelete
  6. Hata katika maisha ya kila siku ni vizuri tusichukulie hivihivi uhai, amani, utengamano na mafanikio yetu bali tushukuru Mungu kwa kila jambo. Kumweka Mungu mbele katika mikakati yenu na kushukukuru kwa mafanikio ni jambo zuri sana.

    ReplyDelete
  7. Tatizo hamna, wameamua hivyo na benki yao sasa nyie kelele za nini?

    ReplyDelete
  8. Benki ya CRDB hufanya misa za shukrani kupitia dini mbali mbali za wafanyakazi wake na sio KKKT tu kama unavyodhaniwa. Katika misa hizo wafanyakazi wote hukaribishwa bila kujali imani zao.Nadhani wote mnakumbuka sala ya Shukrani ya wafanyakazi waislamu iliyofanywa mwanzoni mwa mwaka kupitia masheikh wa Dar es Salaam. Hakuna ubaya kwa wafanyakazi kumshukuru Mungu kwa kupitia imani zao.Tupige kazi ili tujenge taifa.

    ReplyDelete
  9. Leo ndio nimeamini wengi hawana akili au hawataki kuumiza akili, Una lalamika hapa je umejiuliza labda uenda CRDB walishafanya tayari ukwa dini nyingine???

    Na wakifanya ibada kwa dini hizi 2 uzijuazo wewe wakitokea watu wa dini zingine mtaenda kuabudu huko pia?? Wapo indu sijui, Freemason, nk

    Wanasema anayefikiria Ubaguzi bila kutafakari basi ujue yeye mwenyewe ni mbaguzi...

    Tanzania tuwe wamoja hacheni tofauti za udini au kufikiria kwamba umeonewa kila mara.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...