Makamishna wa Jeshi la Polisi wanaohudhuria mkutano wa mwaka wa maofisa waandamizi wa jeshi la polisi mjini Dodoma wamefurahishwa na matumizi ya teknolojia katika utoaji wa huduma za kifedha.

Makamishna wengi waliofika kwenye banda maalumu la NMB lililopo nje ya ukumbi wa mikutano wa St.Gasper mjini Dodoma ambapo kikao cha mwaka cha maafisa wa polisi kinaendelea, walifurahishwa na uharaka wa kutoa na kuweka fedha kupitia NMB wakala ambapo kupitia teknolojia ya Max Malipo, mteja anaweza kutoa na kuweka fedha na pia kupata huduma zingine za kibenki ambazo angeweza kuzipata katika tawi lolote la NMB.

Wajumbe wa mkutano huo wa polisi walifarijika kuona kuwa siyo lazima kwenda kwenye matawi ya NMB ili kupata huduma za kutoa na kuweka fedha na kufagilia kuwa huduma hizo zilizowekwa nje ya ukumbi wa mkutano zimewapunguzia adha ya kwenda mjini kutafuta huduma za kifedha.
Makamishna wa Jeshi la Polisi,Paul Chagonja na Thobias Andengeye wakijaziwa form maalumu itakayowaruhusu kupata taarifa fupi za akaunti zao za NMB kupitia mtandao wa E-mail kutoka kwa Meneja Mwandamizi katika kitengo cha wateja binafsi,Suzan Shuma huku Daudi Sanga kutoka NMB Dodoma kitengo cha Chap Chap Instant Account akijiandaa kutoa maelezo juu ya huduma ya kufungua akaunti ya chap chap.
Meneja Mwandamizi katika kitengo cha wateja binafsi,Suzan Shuma akimjazia Kamishna wa Polisi kutoka makao makuu ya jeshi la Polisi,Paul Chagonja fomu itakayomruhusu kupata taarifa fupi za akaunti yake ya NMB kupitia mtandao wa E-mail (E-statement).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...