Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Huyu jamaa asemi ni jinsi ghani hawa jamaa wamepataje utajiri(Msingi wa utajiri). Yeye anaelezea tu jinsi watu wanavyochagua jinsi ya kutumia pesa yao. Kwanza anasema, watu masikiani wananunua vitu wasivyoiitaji, ambavyo si kweli. Je maitaji ya msingi kama kulipa kodi ya nyumba, umeme, malazi, ushuru, chakula n.k siyo maitaji? Kwanza aeleze ni jinsi ghani mtu anapata utajiri. Nachojua watu wanamiliki mali(mfano wamepewa, wameachiwa), Wameenda shule na wakawa na bahati wakapata kazi inayolipa vizuri. Wengine wamezaliwa na vipaji, mfano, Bill Gates alipogundua mtandao, au wasanii na wanamichezo mbali mbali. Mtu anaweza kushinda bahati nasibu akawa tajiri hapo hapo. Na njia ya mwisho ni Wizi na ujambazi, ambao ndiyo umewafanya mataifa makubwa matajiri kwani waliwatumia watumwa na kuiba rasimali za mataifa ya Kiafrika kujitajirisha. Na hapo hapo tunaona viongozi wa kiafrica wanavoiba rasimali za watu kujitajirisha. Hii system ni mbovu kabisa, kwanza mfano anaotumia wa "Baba tajiri na baba Masikini"-ukienda pale wanataka mtu uende ukawashawishi wenzie waje wauze vitu vayo. Ni kama Pyaramid scheme- haikupi utajiri.

    ReplyDelete
  2. Mdau wa kwanza hapo juu swali lako ni la msingi, ila maelezo yaliyoko kwenye hii videoclip hayatatosheleza kiu yako. Moja ya sehemu za kupata majibu yako soma kitabu cha "The Richest Man in Babylon" kilichoandikwa na George Samuel Clason. Nafikiri kimetafasiriwa kwa kiswahili na kiko nadukani hapa nchini.

    Kwenye kitabu hicho ndipo unapoona jinsi gani nidhamu inahitajika katika kuutafuta utajiri, kama kweli unauhitaji huo utajiri! Maana sio kila mtu anataka kurundika mapesa kuhesabika uko juu kwenye ligi ya matajiri wakubwa!

    Iulize nafsi yako kama uko tayari kuingia kwenye hiyo ligi, au la hasha, kwamba unaridhika ni kipato cha kutoshereza mahitaji na starehe zako za msingi!

    Maana kwa kutaka kurundika mipesa kwa gharama yoyote ile ili uonekane kwenye jamii kuwa wewe ni kidume, ndio inapelekea kutumia njia zozote za wizi, ubadhilifu, uchakachuaji ili tu upate "super profit". Wengine wanauza hata vitu visivyofaa kwa maisha ya binadamu na mazingira yake, ili mradi tu atunishe mfuko wake!

    Na katika kitabu nilichotaja hapo juu, ndipo utakapojua kuwa huwezi kuupata utajiri kwa kuajiriwa, labda umuibie mwajiri wako!!

    ReplyDelete
  3. Mijitu mingine bana inakurupuka tu, mtandao aka world wide web haukugunduliwa na Bill Gates, bali uligunduliwa na mwingereza
    Sir Timothy John "Tim" Berners-Lee, OM, KBE, FRS, FREng, FRSA, DFBCS- mwezi Novemba 1989.
    Bill gates hakuzaliwa na kipaji, bali he worked very hard in his field, at some point he used to have sleepless nights in the computer science departments in seattle.

    ReplyDelete
  4. Mchangia Mada hapo kwanza hapo juu naona hujaelewa somo kabisa, angalia hiyo video upya. Cha msingi ni ku adopt formula ya kupata zaidi, hajasema usilipe umeme au usiwe na gari au usiwe na nyumba. yeye kasema uwe opportunist. kaonyesha how matajiri wanazidi kuwa matajari sababu wana nunua asset zinazo walipa, so hata wewe unatakiwa ufikirie hivyo, badala ya kununua magari 5 nunua mmoja then hizo hela za gari tani invest kwenye money generating projects.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...