Shirika lisilokuwa la kiserikali linalojihusisha na uhifadhi wa mazingira na wanyama pori la World Wide Fund for Nature (WWF), limejiunga katika jitihada za kitaifa na kimaifa za kupambana na ujangili nchini ambapo pamoja na mambo mengine limetoa mabango yanayotahadharisha wananchi na wageni waingiao na watokao Tanzania kutojihusisha na shughuli yoyote inayohusiana na ujangili wa wanyama.

Akikabidhi vifaa hivyo Novemba 27, 2014 jijini Dar es Salaam kwa Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wa jijini Dar es salaam ,Bw.Moses Malaki,Mkurugenzi wa WWF Tanzania Bw. Bell'Aube Houinato,aliwataka jumii ya za ndani na za kimataifa kuhakikisha zinaongeza jitihada ili kuhifadhi rasilimali hizo kwa manufaa ya sasa na kizazi kijacho.

" Jukumu la kumaliza kadhia hii ya biashara haramu ya nyara za umma ni la wote si la serikali pekee au WWF bali umma mzima wa Tanzania na kimataifa,hivyo kila mmoja kwa sehemu yake na eneo lake awajibike ipasavyo",alisema Bw.Houinato.

Aidha,aliongeza kuwa ni jukumu la kila mmoja wetu kuhakikisha vyombo vinavyohusika na ulinzi na uangalizi wa rasilimali zetu vinajengewa uwezo wa kimaarifa na kivifaa ili kuhakikisha vyombo vyote vinatimiza wajibu wake kwa tija kubwa.

Kwa miaka ya hivi karibuni nchini Tanzania,kumeibuka tatizo la ujangili ambapo mauaji a Tembo na Faru yameongezeka huku jitihada za kimataifa na kitaifa zikiwa zinaonekana kulegelega jambo lililozishtua jamii za kimataifa hivyo kujiunga na kuongeza bidii katika vita hiyo.
 Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wa jijini Dar es salaam ,Bw.Moses Malaki (kulia), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), wakati wa hafla ya kukabidhiwa mabango yanayotahadharisha wananchi na wageni waingiao na watokao Tanzania kutojihusisha na shughuli yoyote inayohusiana na ujangili wa wanyama (kushoto), Mkurugenzi wa WWF Tanzania Bw. Bell'Aube Houinato.PICHA NA PHILEMON SOLOMON
 Mkurugenzi wa WWF Tanzania Bw. Bell'Aube Houinato akisisitiza jambo kuhusiana na vyombo vinavyohusika na ulinzi na uangalizi wa rasilimali za nchi.
 Waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wa jijini Dar es salaam ,Bw.Moses Malaki (meza kuu kulia), wakati wa hafla hiyo.
 Mkurugenzi wa WWF Tanzania Bw. Bell'Aube Houinato (kulia), akimkabidhi Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wa jijini Dar es salaam ,Bw.Moses Malaki moja ya mabango hayo.
 Muonekano wa moja ya mabango hayo yenye luga tatu ambayo yatawekwa sehemu mbalimbali ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wa jijini Dar es salaam.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...