Na Andrew Chale, Bagamoyo

CHAMA Cha Afya ya Jamii Tanzania (Tanzania Public Health Association-TPHA), kipo kwenye mkakati kabambe wa kuendeleza na kuinua mapato ya chama hicho ikiwemo kujenga jengo la kitega uchumi la kisasa litakalo kuwa na zaidi ya gorofa 20, katika makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam.

Hayo yalibainishwa mjini hapa jana kwenye kongamano la 31 la Kisayansi na Mkutano mkuu wa mwaka wa TPHA unaoendelea katika ukumbi wa Stella Maris, mjini Bagamoyo ambapo wataalamu wa majengo nchini wa kampuni ya K&M Archplans (T)Ltd, walipowasilisha mpango kazi wao huo ikiwemo mchoro wa jengo hilo la TPHA litakavyokuwa.

Wataalamu hao wa K&M Archplans, kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Profesa Arch Livin Mosha alisema kampuni yao imebobea katika ukandarasi wa majengo mbalimbali ikiwemo kuwa na uzoefu wa kutosha katika usanifu na mpanilio wa majengo. Jengo hilo linatarajiwa kujengwa makao makuu ya TPHA, yaliyopo Kinondoni, Victoria Makumbusho, jijini Dar es Salaam.

Naye Mwenyekiti wa TPHA Taifa, Dk.Elihuruma Nangawe alieleza kuwa, Chama hicho kitaendela na mchakato wake ikiwemo kujadiliana kwa kina na wanachama katika kufikia malengo ya utekelezaji wake ambapo mpango wa TPHA kuwa na jengo la kisasa la gorofa 10 ama 25 ambapo itategemea na mchakato wake.

Naye Katibu Mtendaji wa TPHA Taifa, Dk. Oberlin Kisanga alisema kongamano hilo ni la kuwakutanisha wataalamu ili kubadilishana ujuzi, uzoefu na kutoa mapendekezo namna ya kuleta mabadiliko katika jamii hususani sekta ya afya hapa nchini. Kongamano hilo la kisayansi lililoanza Jumatatu ya Novemba 24, wiki hii, linatarajia kumalizika Ijumaa ya Novemba 28 wiki hii.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya K&M Archplans (T) Ltd, Profesa Arch Livin Mosham akifafanua jambo juu ya jengo hilo la kisasa linalotarajiwa kujengwa na TPHA (Linaloonekana kushoto kwake pichani), kwa wajumebe wa mkutano huo (Hawapo pichani) juzi, katika kongamano la 31 la kisayansi na mkutano mkuu wa mwaka, unaoendelea, katika ukumbi wa Stella Maris, Mjini Bagamoyo, Pwani.
Mkurugenzi wa K&M Archplans (T)Ltd, Arch Albert Mwambafu akifafanua jambo kwa wajumbe wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (Tanzania Public Health Association-TPHA), (Hawapo pichani) wakati wa kongamano la 31 la Kisayansi na Mkutano mkuu wa mwaka wa TPHA unaoendelea katika ukumbi wa Stella Maris, mjini Bagamoyo. ambapo jengo ni mradi wa kuinua mapato ya TPHA kwa ajili ya kuendelea kuelimisha jamii kuhusiana na mambo ya afya.
Katibu Mtendaji wa TPHA Taifa, Dk. Oberlin Kisanga akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa TPHA, akiwemo Dk. Anna Nswilla (Treasure of TPHA), (katikati) akifuatiwa na Dk.Faustine Njau (TPHA Life Member).
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya K&M Archplans (T) Ltd, Profesa Arch Livin Mosha (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa TPHA Taifa, Dk.Elihuruma Nangawe, mara baada ya kuwasilisha mada na kuonesha shughuli za kitaalamu za usanifu wa nmajengo hapa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...