Wadau wa Kundi la Kandanda katika Mtandao wa kijamii wa Facebook ambao leo wamekutana pamoja katika kusherehekea maadhimisho ya miaka minne ya Kundi hilo,kwa kusakata mtanange mkali sana katika Uwanja wa TCC Club,Changombe jijini Dar es Saalam.Mtanange huo ulizikutanisha timu mbili zilizoundwa na wadau Dizo Moja na Ismail.TeamDizo iliibuka kidedea kwa kuinyuka TeamIsmail mabao 4-1 bila huruma na kufanikiwa kutwaa kombe la shampeni.
 Muanzilishi wa Kundi la Kandanda ndani ya Mtandao wa kijamii wa Facebook,Patrick Dumulinyi (wa pili kulia) akikabidhi kombe la ubingwa kwa Nahodha wa TeamDizomoja,Husolin Ulomi baada ya kuishinda TeamIsmail mabao 4-1 katika mtanange wa kuadhimisha miaka minne ya kuanzishwa kwa kundi hilo,leo kwenye Uwanja wa TCC Club,Chang'ombe jijini Dar.
 Muanzilishi wa Kundi la Kandanda ndani ya Mtandao wa kijamii wa Facebook,Patrick Dumulinyi. 
 Beki wa TeamIsmail akichambuliwa na Beki wa TeamDizomoja wakati wa mchezo wa kuadhimisha miaka minne ya kundi la Kandanda ndani ya Mtandao wa Facebook,uliochezwa asubuhi ya leo kwenye Uwanja wa TCC Club,Chang'ombe jijini Dar es Salaam.
 Mshambuliaji wa TeamIsmail,Majaliwa Mkinga (kushoto) akionyesha ufundi wake mbele ya Beki wa TeamDizomoja katika mchezo uliopigwa leo kwenye Uwanja wa TCC,Chang'ombe jijini Dar.hadi mwisho wa Mchezo TeamDizomoja iliibuka kidedea kwa ushindi Mnono wa Mabao 4-1.

Super Sub wa TeamIsmail,Nassor Binslum akimtoka mchezaji wa TeamDizomoja,Damas.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. hongera sana Patrick Dumulinyi my ex workmate enzi za zantel.
    its Jacque

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...