Mtaalamu wa masuala ya lishe na Afya ya jamii kutoka taasisi ya Footprint,Allan Rwechungura akiongea na viongozi wa Wilaya ya Monduli juu ya matumizi ya vyakula vilivyoongezewa virutubishi.Kampeni ya kuhamasisha matumizi a vyakula vilivyoongezewa virutubishi vijijii inaendelea katika wilaya mbalimbali nchini.
Viongozi wa kabila la Wamasai maarufu kama ‘Malaigwanani” wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa wataalamu wa masuala ya lishe kutoka wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakati wa semina ya uhamasishaji wa matumizi ya vyakula vilivyoongezewa virutubishi vijijini iliyofanyika wilayani Monduli,mkoni Arusha leo.
Viongozi wa kabila la Wamasai maarufu kama ‘Malaigwanani” wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa wataalamu wa masuala ya lishe kutoka wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakati wa semina ya uhamasishaji wa matumizi ya vyakula vilivyoongezewa virutubishi vijijini iliyofanyika wilayani Monduli,mkoni Arusha leo.
Viongozi wa kabila la Wamasai maarufu kama ‘Malaigwanani” Katika picha ya pamoja na wataalamu wa masuala ya lishe kutoka wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Taasisi ya FootPrint baada ya semina ya uhamasishaji wa matumizi ya vyakula vilivyoongezewa virutubishi vijijini iliyofanyika wilayani Monduli,mkoni Arusha leo.
Viongozi wa kabila la Wamasai maarufu kama ‘Malaigwanani” wakipata nyama choma baada ya semina ya matumizi ya vyakula vilivyoongezwa virutubishi iliyotolewa na wataalamu wa masuala ya lishe kutoka wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Taasisi ya FootPrint wilayani Monduli,mkoni Arusha leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Fanyeni utafiti wa kutosha kabla ya "kuimba" kuhusu vyakula kuongezwa virutubishi! Kwa Amerika ambako wametumia sana vyakula hivi madhara yake yameshaanza kuonekana, sio tu kwa ardhi na viumbe vya mashambani, bali pia kwa afya za binadamu. Ukiingia mitaani huko majuu utashangaaa jinsi watu walivyonenepeana kwa ajili hiyo!

    Hapa kwetu ardhi yetu hijachafuka sana kuifanya ikashindwa kutoa mazao yenye virutubishi vya asili! Tutaichafua tu tukianza kuwa na chakula kama hicho kinachoongezewa virutubishi!

    Ni bora kuepusha janga linaloweza kutokea kwa vyakula kama hivi. India wameaanza kampeni kubwa ya kupinga jambo hili. Sisi hapa Afrika tusiwe tukawa kama "dodoki" alilosema Mwl Nyerere, kuzoa kila kitu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...