Na Benedict Liwenga na Magreth Kinabo.

RASIMU ya Katiba  Mpya  iliyopendekezwa inatarajiwa  kuwasilishwa  katika Bunge Maalum la Katiba Septemba 24, mwaka huu.

Mabadiliko hayo yametangazwa leo jioni na Katibu wa Bunge Maalum la Katiba, Yahya Khamis Hamad wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Aidha Katibu huyo amesema uamuzi wa mabadiliko hayo, umetokana na kufanyika kikao baina ya Kamati ya Uongozi wa Bunge hilo na Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi. 

Hata hivyo Katibu huyo amesema kuwa kazi ya uandishi wa Rasimu hiyo imeshakamilika na kazi iliyobakia ni kuipitia kwa makini, hali iliyosababisha mabadiliko ya uwasilishaji wa Rasimu hiyo katika Bunge hilo, uliopangwa kufanyika hapo kesho Septemba 22, mwaka huu.

“Uwasilishwaji wa Rasimu ya Katiba inayopendekezwa sasa utafanywa siku ya Septemba 24, mwaka huu, ” alisema Katibu wa Bunge hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Sijapata muda wa kuisoma rasimu ya tume ya Jaji Warioba, lakini nimeiona katika mtandao wa Jamii Forums. Bado sijaisoma.

    Nilisikia kuwa rasimu ile ya tume ya Jaji Warioba ilikuwa kwenye tovuti ya tume ile, lakini iliondolewa. Sijui ni nani aliyeiondoa.

    Ni jambo zuri watu wapewe fursa ya kuiangalia ile rasimu ya tume ya Jaji Warioba, sambamba na hii itakayowasilishwa Bungeni siku chache zijazo.

    Hii itasaidia kuthibitisha au kukanusha madai kuwa rasimu ya tume ya Jaji Warioba imechakachuliwa. Hii dhana imejengeka sana katika jamii, na wahusika wangefanya vizuri kuziweka zote mbili, zisomwe moja sambamba na nyingine. Huu ndi ushauri wangu.

    ReplyDelete
  2. Wala hakuna ramri hapa kinachopendekezwa no rasimu ya Katiba ya CCM ni juu ya wananchi kukubali Kuwa hayo ndo maoni yao au Yale ya tume ya warioba

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...