Mkuu wa wilaya ya Makete mh Josephine Matiro akizungumza katika kikao hicho.
Wananchi waliozaliwa wilayani Makete mkoani Njombe ambao wanaishi nje ya wilaya hiyo, wameshauriwa kuipenda wilaya yao kwa kuja kuwekeza pamoja na kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo ndani ya wilaya hiyo
Rai hiyo imetolewa hii leo na Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro katika kikao baina yake na wananchi wa Makete waishio jijini Dar es Salaam kilichofanyika jijini humo
Katika kikao hicho mkuu wa wilaya amewashirikisha mambo mengi ya kimaendeleo katika wilaya ya Makete ikiwemo uwepo wa shule ya sekondari ya wasichana ya Makete Girls secondary ambayo pamoja na kuanza kufanya kazi bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali
Mh. Matiro amezitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na ukosefu wa bweni na kuwa wanafunzi wanalala kwenye vyumba vilivyojengwa kwa ajili ya madarasa, bwalo, jiko pamoja na maabara ambavyo vinatakiwa viwepo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...