Baadhi ya Wajumbe wanawake wa Bunge Maalum la Katiba wakiimba kwa furaha wakati wa semina iliyofanyika 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba (wa kwanza kulia) akipitia taarifa ya mapendekezo ya mtandao wa wanawake na Katiba Tanzania wakati wa semina iliyofanyika 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma.
Mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Bi. Usu Mallya akitoa mada kuhusiana na suala la kijinsia katika Katiba, wakati wa Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma. (Picha zote na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Katiba yenye Mrengo wa Jinsia?? Hii yote ni siasa tu! Ukishajali haki za binadamu ndani ya katiba na ukaifanyia kazi, huna haja ya kuwa na mambo mengine, eti haki ya wanawake, watoto, walemavu, n.k.

    Ukiheshimu haki za binadamu bila kujali jinsia, rangi, elimu, umri, kabila, utakuwa umepunguza utitili wa makundi yanayoongeza gharama za uendeshaji wakati kunakuwa hakuna tija!!

    Cha msingi ni kuondoa vichwani mwetu kitu kinaitwa "mfumo dume" tu! Mfume dume umeiua hii Dunia yetu, kwenye ngazi zote. Na kwa undani wanaume bado tunaogopa nguvu ya wanawake siku wakiamka na kujitambua kuwa wana uwezo mkubwa kuliko wanavyochukuliwa!

    Hata kwa baadhi ya dini kuna harakati nyingi za kuwaacha nyuma wanawake kwenye majukumu mengi tu ya uongozi!

    Ninachowaomba Wanawake wasije wakataka kulipiza, bali wautumie huo uwezo wao kwa kile kilichokusudiwa - maisha bora kwa kila kiumbe duniani!!

    Wanaume???? Jiandaeni kwa mabadiliko!!

    mujwahuki
    kashonge.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...