Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Mtongani alitoa maoni yake juu ya kura iliyopigwa na wananchi wa Scotland kuunga mkono Muungano dhidi ya wale waliotaka kujitenga.

Kinana alisema amekuwa akipigiwa simu siku nzima na waandishi wa habari kutaka kusikia maoni yake juu ya kura iliyopigwa Scotland.

Wananchi wa Scotland wamepiga kura na kuunga mkono muungano wa miaka 307 baina ya nchi hiyo na Uingereza katika kura ya maoni ya kihistoria iliyokuwa ikisubiriwa kuamua iwapo Scotland itajitenga.

“Watu wa Scotland wamezungumza. Tumechagua umoja dhidi ya mgawanyiko na mabadiliko chanya kuliko mgawanyiko usio na maana”.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Achaneni na mambo ya Scotland hawa ni watu ambao siyo matajiri lakni neno njaa na kukosa mahali pa kulala hawalijui ndiyo maana wameaanzisha hiyo madness tu discus mambo yetu muhimu na jinsi ya kupunguza matatizo kama mjini hakuna maji mishahara ya asii mia 95 ya watanzania hayakidhi mahitaji ukifaulu huna pesa University utaisikia jina na mengineyo mengi ambayo yanaweza kujaza more than 10 pages msimuulize Kinana maoni yeye siyo Mscotish wala siyo Muingereza kwa hiyo sidhani kama maoni yake yatawasaidiamuulizeni Gordon Brownambaye waingereza walikuwa hawamtaki kwa vile ni mscotish lakini na yeye anaunga mkono muungano kwa sababu za maana.Kuvunjika kwa Muungano nafikiri Wabunge wote wangekuwa hawana kazi na mengineyo mengi kwa watu wa ngazi za juu yangewaathiri Big time Hebu tujikubushe kidogo kuanguka kwa Taifa la Kisoviet Gobachev alijikuta jobless.Cha muhimu wakumbusheni Wazanzibar wakivunja Muungano wata waaribia watu unga mawaziri nk wawakilishi wata Win naCUF itatawala Bara hatuna noma Tuna Bunge moja tu

    ReplyDelete
  2. Ancal hata mimi sipendelei muungano uvunjike naamini wazanzibar wengi hawapendi muungano usiwepo wanacholalamika muungano uboreshwe uondoe matatizo yanayolalamikiwa hasa bidhaa zinaotoka znz kuja bara zinalipishwa mara mbili na tra znz ipo na bara ipo ni moja na wazanzibar wengi niwafanyabiashara tatueni hili maneno yatapungua

    ReplyDelete
  3. scotland wanafanya kura ya maoni mara ya tatu sasa na ya nne itafanyika hawajui kama miaka mitano kumi au kumi na tano na washajua kuwa ikifanyika hiyo hakuna muungano kwa sababu asilimia wanaotaka kujitenga ilianza 25 35 na juzi 45 sasa ccm leteni kura ya maoni tanzania kuhusu muungano wetu wananchi ndio waamue sio vyama vya siasa hiyo sio demokrasia demokrasia ndio hiyo ya scotland msijaribu kuiga kwa vigezo vya ubabaishaji KURA YA MAONI NDIO JIBU KAMA WANAVYOFANYA WANA DEMOKRSIA WOTE ULIMWENGUNI.

    MDAU.
    ENGLAND.

    ReplyDelete
  4. Wewe Mdau wa 3 hapo juu NINYI NDIO WALEWALE , Kura ya Maoni wameshindwa Wascotch huko Uingereza na Wameumbuka juzi mtaweza ninyi wa Mchamba wima Zanzibari?

    Hata na ninyi tukipiga Kura za Muungano hapa Tanzania ni 100% mtashindwa !!!

    ReplyDelete
  5. Mimi ninaomba na Tanzania tupige hizo Kura za Muungano ili wale wa UKAWA na Wapinga Muungano watakapo shindwa kama wenzao huko Scotland-UK juzi tukate mzizi wa fitna ili tupate muda wa kufanya mengine na sio mabishano kama Muungano unafaa au haufai!

    ReplyDelete
  6. Kinachonikera mimi kwenye Muungano huu ni Wabunge wa Zanzibar kukaa kwenye Bunge la budget mwanzo mpaka mwisho wanajadili budget za wizara zingine ambazo sio za muungano, zinawausu nini. Wanakula posho za Tanganyika bure na kutuongezea matumizi yasiyo ya lazima. Waje kujadili wizara za muungano tu wakimaliza warudi kwao. Plili Mtanganyika akifanya kazi Zanzibar akinunua kitu kama gari, tv, sofa n.k. siku ya kurudi nyumbani analipia kodi wakati akiwa kazini Zanzibar alikuwa anakatwa PAYE kwenye salary na zinaingia TRA. Mimi mwenyewe nimefanyiwa hivyo na nilikaa Zanzibar 5yrs.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...