Na Editha Karlo, Kigoma 
ZAIDI ya Tani 24 za vyakula,dawa za binaadam na vipodozi zimeteketezwa na mamlaka ya chakula na dawa(TFDA)katika mikoa minne ya kanda ya katikwasababu ya kutofaa kwa matumizi ya binaadam. 
 Akizungumza wakati wa zoezi la uteketezaji wa bidhaa hizo zilizokamatwa katika zoezi la kustukiza ndani ya Manispaa ya Kigoma ujiji Mkoani hapa Mkaguzi wa TFDA kanda ya kati Engliber Bilashoboka alisema kuwa bidhaa hizo zilikamatwa kati ya Julai mwaka jana na Juni mwaka huu.
 Bilashoka alisema kuwa kuteketezwa kwa bidhaa hizo kunatokana na ukaguzi unaofanywa na maofisa wa TFDA katika mikoa mbalimbali nchini na lengo likiwa ni kuondoa sokoni bidhaa zilizoisha muda wake na zisizofaa kwa matumizi ya bindaadam 
 Alisema pia kufuatia zoezi hilo mamlaka yake imekifungia kiwanda cha mikate cha Kigoma bekari baada ya kukutwa na tani 1.5 za mikate mibovu, pamoja na machinjio ya ujiji kwa kufanya shughuli zake katika hali inayotishia afya za wananchi 
 Alisema bidhaa hizo zimekamatwa katika mikoa ya Tabora,Kigoma,Singida na dodoma alisema kuwa katika bidhaa zilikamatwa na kuteketezwa nyingi zilikuwa zikiuzwa huku muda wake wa kuwa sokoni ukiwa umeisha na zingine zimepigwa marufuku kuuzwa nchini. Ofisa huyo alisema kuwa uteketezaji katika manispaa ya kigoma kwa muda wa wiki moja mpaka sasa ,alisema mamlaka ya ke imeteketeza zaidi ya tani 4.1zenye thamani ya shilingi milioni 24 ambavyo havifai kwa matumizi ya binaadamu Naye Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Moses Welansari akizungumzia zoezi hilo alisema kuwa wamekuwa wakikutana changamoto za wenye maduka zilizokatazwa au zilizoisha muda wake wa matumizi. 
 ''Elimu imekuwa ikitolewa kwa wafanyabiasha mara kwa mara ili kuepuka kuweka sokoni bidhaa zisizotakiwa na mamlaka za serikali na zilizoisha muda wake ''alisema Kaimu Mkurugenzi
 Shehena tani 1.5 ya mikate mibovu kutoka Kigoma Bakery  ikishushwa kwenye dampo la Businde Mkoani Kigoma tayari kwa kuteketezwa kutokana na kutofaa kwa matumizi ya binadam shehena hiyo imebambwa kufuatia msako wa kushitukiza wa (Mamlaka ya chakula na dawaTFDA)
 Zaidi ya tani moja na nusu za dawa binadaam kutoka duka la Mambo Leo la mjini kigoma zimeteketezwa na TFDA baada ya kuonekana hazifai kwa matumizi ya bindaadam
Bidhaa mbalimbali za madukani zikiwa tayari kwaaajili ya kuteketezwa baada ya muda wake wa matumizi kuisha,kufuatia msako wa kushitukiza wa TFDA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ndo tutapona kweli kwa hali hiiiiii?????

    ReplyDelete
  2. JE HAWA WAMECHUKULIWA HATUA GANI? KILA MARA NAONA TFDA WANAKAMATA MADAWA NA VYAKULA VIBOVU KWA AFYA YA BINADAMU ILA SIJASIKIA WAKIFUNGWA AU HATA KUTOZWA FAINI KUBWA ILI IWE FUNZO KWA KUCHEZEA AFYA ZA WATANZANIA.......LAKINI KIMYA. MWENYEKITI WA CCM DAR ES SALAAM RAMADHANI MADABIDA ALIANDIKWA KWENYE MAGAZETI AKIUZA MADAWA FEKI YA UKIMWI LAKINI LEO YUPO ANADUNDA MITAANI TU HAKUNA KINACHOENDELEA. JE MBONA HATUONI WATU WAKIFUNGWA KUTOKANA NA MAKOSA HAYO MAKUBWA YA KUUA WANANCHI? NAOMBA NIELEWESHWE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...