Na Sifa Lubasi, Kongwa
HALMASHAURI nchini zimetakiwa kununua nyumba za bei nafuu zinazojengwa na Shirika la Nyumba (NHC) ili kuwapangisha watumishi wake.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akifungua mradi wa nyumba nafuu katika eneo la Mnyakongo wilayani Kongwa mkoani Dodoma.

Alisema kumekuwa na tabia ya baadhi ya maeneo watumishi wa halmashauri kukaa mbali na sehemu zao za kazi kwa visingizio vya kukosa makazi.

Alisema sababu hiyo sasa haina msingi katika maeneo ambayo NHC imejenga nyumba zao kwani halmashauri inaweza kununua nyumba hizo na kuwapangisha watumishi wake.

‘’ Hawa NHC wana utaratibu kwa kupitia mabenki wanayoshirikana nayo hivyo kwa kutumia utaratibu huo halmashuri mnaweza kwenda katika hizo benki na kuingia mkataba na kukopa nyumba hizo na kisa kuwapangisha watumishi…’’ alisema.

Aidha Rais Kikwete alisema shirika hilo linafanya kazi nzuri katika ujenzi wa nyumba hizo za bei nafuu huku akilitaka kuongeza zaidi idadi ya nyumba. Alisema ni vyema sasa halmashuri zikaongeza maeneo ya kujenga nyumba hizo ili wananchi wengi zaidi waweze kuishi katika nyumba bora.

Akizungumza katika ufunguzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa NHC Nehemia Mchechu alisema mradi huo ni utekelezaji wa mpango wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu. Alisema mradi huo wenye nyumba 44 hadi kukamilika utakuwa umegharimu Shilingi bilioni 1.2.

Alisema nyumba hizo zinauzwa kwa gharama kati ya Sh milioni 35 hadi 40 kulingana na ukubwa wa nyumba husika.

Hata hivyo alisema bado kuna tatizo la kodi katika uuzaji wa nyumba hizo na ndio kinachofanya kuuzwa kwa bei kubwa.

Alimuomba Rais kusaidia katika kusukuma nia ya kushusha kodi ili nyumba hizo ziuzwe kwa bei nafuu na kila mwananchi aweze kununua.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kuashiria ufunguzi mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma wanaoshuhudia ni pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Tuguluvala Simbachawene na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia jiwe la msingi mara baada ya kufungua mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma wanaoshuhudia ni pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Tuguluvala Simbachawene na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Tuguluvala Simbachawene na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, Waziri wa Ujenzi Dk John Pombe Magufuli na Mbunge wa Afrika Mashariki Adam Kimbisa.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza katika hafla hiyo jana
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai akizungumza katika hafla hiyo jana
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu wakati akitembelea mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma. Mradi huo una jumla ya nyumba 44.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...