WATU kumi wakiwemo watoto wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine saba wamejeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha magari mawili.

Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa nne asubuhi ikihusisha gari ndogo ya abiria maarufu daladala lenye namba za usajili T 237 BFB aina Toyota Hiace na gari kubwa aina ya Fuso lenye namba za usajili T 158 CSV.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wamesema ajali hiyo ilitokea maeneo ya Mbalizi baada ya Hiace iliyokuwa ikitokea Mbeya mjini kuelekea Mbalizi kulivaa Fuso ilikuwa ikiingia barabarani.

Walisema inasemekana dereva wa Hiace gari yake ilimshinda kutokana na kutelemka mlima mkali wa Mbalizi inagawa pia walimtupia lawama dereva wa Fuso ambaye alikuwa akiingia barabarani bila kuchukua tahadhari.

Muuguzi Mkuu wa Hospitali teule ya Ifisi Mbalizi, Sikitu Mbilinyi, ambako Majeruhi na marehemu walikimbizwa hapo alithibitisha kupokea majeruhi 7 ambapo alisema kati yao ni wanawake 3 na wanaume 4.

Alisema kati ya majeruhi hao wawili wamepewa rufaa kwenda hospitali ya Rufaa Mbeya kutokana na kuhitaji msaada zaidi huklu wengine wakiendelea kupatiwa msaada wa haraka ili kunusuru hali zao.

Mbilinyi aliongeza kuwa pia wamepokea miili ya marehemu 10 wakiwemo watoto wawili na Wanawake wanne na Wanaume wanne.

Hata hivyo majina ya majeruhi na marehemu hayajaweza kupatikana mara moja kutokana na kuwa katika hali mbaya ambapo Dereva wa Fuso akitokomea mara baada ya tukio. NA MBEYA YETU BLOG
Hivi ndivyo ambavyo Daladala hiyo ilivyojibamiza muda mchache uliopita. 
Gari hilo aina ya Tata likiwa limepaki pembeni Muda mchache baada ya kupata ajali hiyo
Askari wa usalama wa Barabarani akiwa anatazama na kuchunguza zaidi ajali hiyo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Uzembe wa madereva unamaliza watu Mbeya. Sumatra fuatilieni leseni za madereva wengine hata hawafai kuwa madereva. Too much is harmful. Tumechoka kusikia mambo ya ajali ajali kila siku Mbeya.

    ReplyDelete
  2. Wizara ya usafirishaji au uchukuzi ichukue hatua juu ya janga hili la ajali mkoani Mbeya. Kila kukicha Mbeya ajali kila kukicha Mbeya ajali mbona sehemu nyingine hatusikii uwingi wa ajali kama Mby. Oneni aibu madereva na muogopeni Mungu kwa uzembe mnaofanya wa kuangamiza roho za watu wasio na hatia hasa baadhi ya madereva mkoa wa Mby. Inauma sana kuona kila leo ajali wapi Mby ni aibu sana kwa taifa na ulimwengu. Tunapunguza hadhi ya uzalendo wetu. Kila mambo mabaya ni Africa tu lini tutaonekana kama wengine? vita Africa, njaa Africa, ulozi Africa, miundombinu mibovu Africa na zaidi Tanzania, magonjwa huko huko, elimu duni huko huko, rushwa Africa, lini, lini tutastaarabika? tugeuke jamani sisi sio jiwe ni binadamu tunaweza kubadilika. Moyo wangu unaniuma sana kupoteza roho za watu wasiokuwa na hatia na wako katika kujipatia riziki zao.

    ReplyDelete
  3. 50% ya madereva wa Mbeya wana lesen class B na D.. Na 30% hawana lesen kabisa.. Wakidai msimamiz wa usalama barabaran ni mwanamke na msaidiz wake pia ni mwanamke na kaz zao ni ofisin tuu.. Madereva wenyewe wanasema siku tukikaguliwa 3/4 ya daladala zitasimama kwan lesen zao hazina vigezo.. Tumuombe muhusika aangalie upya uteuz huu, wakague lesen na madereva kwan tutaangamia wote.. Barabara za jijin bajaj zinabeba abiria 5 na Dereva wa 6.. Bodaboda hawapo makin, ajal kila kukicha hapa Mbeya.. Tuhurumien wahusika tafadhal

    ReplyDelete
  4. Jaman Jaman vyombo husika, mpo wap??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...