Aliyekuwa Waziri wa Afya ambaye kwa sasa ni Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Juma Duni Haji akimkabidhi Ripoti Waziri mpya wa Wizara ya Afya Rashid Seif Suleiman katika hafla ya kukabidhiana Ofisi iliyofanyika ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja mjini Zanzibar.
Mkurugenzi Utumishi na Uendeshaji wa Waizara ya Afya Juma Rajab Juma kulia akiwakaribisha Mawaziri wa Afya na Miundombinu katika hafla ya kukabidhiana Ofisi mawaziri hao baada ya kuteuliwa katika nafasi zao hivi karibuni.
Aliyekuwa Waziri wa Afya ambaye kwa sasa ni Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Juma Duni Haji akizungumza na baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Afya katika hafla ya kukabidhiana Ofisi iliyofanyika Wizara ya Afya Mnazi mmoja mjini Zanzibar.
Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman akizungumza na Watendaji wa Wizara hiyo mara baada ya kukabidhiwa Ofisi na Aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Juma Duni Haji. Katika mazungumzo yake aliwaomba kushirikiana naye ili kutimiza malengo ya Wizara hiyo mpya kwake. picha na Abdallah Omar-Maelezo Zanzibar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Waziri wa Afya wa Muungano ni Dr. Rashid Seif Suleiman na Waziri wa Afya wa Zanzibar ni pia ni Mh. Rashid Seif Suleiman !

    Je wakienda nje ya Tanzania kwenye Mikutano watajitofautisha vipi wakiwa wana jitambulisha?

    Au watasema kwa kuwa tuna mahusiano mazuri na Wachina wao Wachina wanafanana sura na sisi Watanzania tuna fanana majina!!!

    ReplyDelete
  2. Nyie haya tuu yayo kwa yayo

    ReplyDelete
  3. Waziri wa muungano ni Dr. Seif Rashid na yule wa Zanzibar ni Dr. Rashid Seif, si kama ulivyo ulivyoainisha hapo juu. Majina yao ni tofaiti.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...