Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akifungua kongamano la siku moja la kupata maoni ya wadau kuhusu rasimu ya sera ya Petroli linalofanyika leo katika ukumbi wa mikutano uliopo Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo limejumuisha wadau wa mafuta na gesi, wabunge, viongozi wa dini na mikoa iliyofanyiwa utafiti wa mafuta na gesi na vyama vya siasa.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro (hayupo pichani) wakati akifungua kongamano la siku moja la kupata maoni ya wadau kuhusu rasimu ya sera ya Petroli linalofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam.
Wakuu wa mikoa ya Mbeya Abbas Kandoro (katikati) na Lindi Ludovick Mwananzila( kushoto) na Mjiolojia Mwandamizi kutoka Idara ya Nishati Adam Zuberi (kulia) wakisikiliza mada ya rasimu ya sera ya Petroli iliyokuwa inatolewa leo katika kongamano la siku moja la kupata maoni ya wadau kuhusu rasimu hiyo lililofanyika leo katika ukumbi wa mikutano uliopo Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Nishati Eng. Hosea Mbise akiwasilisha mada kuhusu rasimu ya sera ya Petroli kwa wadau wa mafuta na gesi, wabunge, viongozi wa dini na mikoa iliyofanyiwa utafiti wa mafuta na gesi na vyama vya siasa wakati wa kongamano la kupata maoni ya wadau lililofanyika leo katika ukumbi wa mikutano uliopo Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa mafuta na gesi, wabunge, viongozi wa dini na mikoa iliyofanyiwa utafiti wa mafuta na gesi na vyama vya siasa wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro (hayupo pichani) wakati akifungua kongamano la siku moja la kupata maoni ya wadau kuhusu rasimu ya sera ya Petroli linayofanyika jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa mkutano (Rapporteur) wakiandika taarifa mbalimbali wakati wa kongamano la siku moja la kupata maoni ya wadau kuhusu rasimu ya sera ya Petroli linayofanyika leo katika ukumbi wa mikutano uliopo Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam. Picha na Anna Nkinda- Maelezo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...