Jana tarehe 29 Julai, 2014 nimefanya mahojiano katika kipindi cha PowerBreakFast kinachorushwa na Clouds FM. Baadhi ya vyombo vya habari vimeandika mahojiano yale. Napenda nitoe ufafanuzi kidogo kuhusu msimamo wangu kuhusu mchakato wa Katiba.

Kwanza, Mimi sijawahi kuwa UKAWA wala kundi lolote lile katika Bunge Maalumu la Katiba isipokuwa kundi linalotaka maridhiano. Msimamo wangu kuhusu Muungano ni Serikali Tatu Zilizoboreshwa (S3z) ili kuwa na Muungano imara usio tegemezi wala egemezi kwa Washirika wake.

Pili, Mimi niliunga mkono ‘protest’ ya baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kupinga lugha za matusi na lugha za kibaguzi zilizokuwa zinaendelea ndani ya mkutano ule. Vilevile niliunga mkono kwamba Rasimu inayopaswa kujadiliwa ni Rasimu iliyotokana na Tume ya Marekebisho ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Sinde Warioba. Nasisitiza umuhimu wa kupata Katiba BORA itakayoimarisha DOLA ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tatu, kwa hali ya sasa kuna mkwamo katika kupatikana kwa Katiba Bora. Mkwamo unaotokana na kutokuwepo kwa nia ya dhati ya kupata maridhiano ya pande zinazopingana. UKAWA hawataki mazungumzo na Viongozi wa Bunge la Katiba badala ya kujenga maridhiano kila siku wanawabeza UKAWA jambo ambalo kamwe haliwezi kujenga mwafaka. Ushauri wangu ni kuahirisha mchakato mzima wa kuandika Katiba mpaka mwaka 2016 baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Katiba ya sasa ifanyiwe marekebisho machache kama ifuatavyo;

i) Tume ya Uchaguzi ili iwe huru na ionekane kuwa huru, ikiwemo kuwaondoa watumishi wa Halmashauri za Wilaya, Miji na Majiji katika kusimamia uchaguzi

ii) Kuruhusu mgombea binafsi

iii) Kuondoa Mafuta na Gesi kama Jambo la Muungano ili Zanzibar ianze mara moja kusimamia kwa uhuru utafutaji wa Mafuta katika vitalu vilivyopo upande huo wa Muungano

Mkutano wa Bunge Maalumu utakaofanyika bila kuwepo kwa maridhiano utakuwa hauna maana yeyote na itakuwa ni sawa na kupoteza muda na fedha za walipa kodi ambazo zingeweza kununua madawa vijijini. Mimi binafsi sitahudhuria mkutano wa Bunge Maalumu kama makundi hasimu hayatakuwa yamefikia maridhiano.

Kabwe Zitto, 
MB/MBMK

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 30, 2014

    Well said,nothing is going to come out of this coming session as long as ukawa is not attending ,the rules are vividly clear that two third total count is required from both mainland and Zanzibar and because theirs no that count from Zanzibar side then this process should be halted till when the two partieshave agreed and all disputes have been settled unless and if the process continues will be wasting tax payer s money for something we all know will not produce results

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 30, 2014

    Asante zitto leo niliposkia umewapinga ukawa nilishtuka lkn leo nimekusoma nimekuelewa hata mm naona bila maridhiano wanaenda kulipata posho tu

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 30, 2014

    This is welcome, fresh, constructive and independent thinking. Bravo Zitto! We need more of this. The official opposition knee-jerk, reactive, predictable thinking have become rather boring and self-serving now. If we can have this plus a break-up of CCM as Mwalimu seemed to wish for at times, then the future of democracy in TZ will be much brighter. Go to sleep CHADEMA and CUF- you thinly veiled religious and ethnic parties; you are the last thing Tanzania needs.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 31, 2014

    Anon wa kwanza get your facts right before you post a comment.
    The truth is two third majority can be opptained without those who walked out (ukawa). As for me i think the whole country must not get hold up by a tiny minority if we truely accept democracy. The bunge must continue.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 31, 2014

    Zito, you are a great thinker

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 31, 2014

    Wabongo wenzangu bwana,
    Ndio nini hii?
    Kujionesha, ubwege au kitu gani?
    Mada iko katika lugha ya Taifa Kiswahili. Wasomaji ni waswahili. Sasa kiingereza kinakusudiwa kuthibitisha nini?
    Kwangu ni kama samaki aliyetayarishwa kimapishi vizuri sana lakini akawa ananuka shombo, haliki.
    Ni matapishi matupu kila nnaposoma mada iliyo katika lugha bora zaidi na yenye wazungumzaji kila pembe halafu wachangiaji mabwege wakatumia lugha ya kigeni.
    Kwa nia ya kujionesha tu.
    Wabongo tuache ubwege. Tuache kujionesha. Vinginevyo hii bongo itaendelea kuwa hivi ilivyo.
    Mndengereko Ukerewe

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 31, 2014

    Zito unatafuta support ya Zanzibar nini? Huna mvuto tena, maswala ya Mafuta upande wa Tanzania Zanzibar kama yapo ktk muungano kwanini ya enguliwe? Basi kama Ni hivo na rasilimali zilizopo Tanzania bara zienguliwe kwenye maswala ya muungano! Na hatima yake hapo hakuna muungano!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...