MAREHEMU MODEST SABINUS KWEKA.
14-04-1968 - 25-07-1999 

Ni miaka 15 leo,tokea ulipotuacha gafla baada ya kuitwa na Mungu Baba wa Mbinguni.Hatuna cha kusema ila ni kushukuru kwa kila jambo Mdogo wetu Modest, tokea hapo maisha ya Familia yetu hayajawa tena mazuri. machache Mungu alitukumbuka lakini kubwa kuliko yote, ni mama yako mzazi ambaye Kansa imemaliza sana, hana tena ziwa, Mguu mmoja na sasa tunakimbilia kukata wa pili. Tunaomba Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema atunusuru na janga hilo.

Unakumbukwa sana na Mkeo Mpenzi Constancia, Mwanao wa pekee Kelvin,Mama yako mzazi Ursula, Ndugu zako

Jane, Festo, Eugenia, Elizabeth, Cecilia, na Thadei;Mashemeji zako wote WaKweka wote wa Narumu, wa Wamallya na Manushi, Wafanyakazi wenzako wa Temeke Hospital wakazi wote wa Temeke Mikoroshini,Ndugu,Jamaa na Marafiki na wote waliokufahamu Misa ya Kumbukumbu Imesomwa mwanza leo Kanisa la Mt. Augustino – Mkolani Mwanza

“Lakini mtu mwema hata akifa kijana atapata pumziko………………………….huyo alionekana amempendeza Mungu, akapendwa naye, hata pindi alipokaa katikati ya wakosaji akachukuliwa.Naye akahamishwa ili uovu usimgeuzie nia yake, wala hila isimdanganye roha yake” Hek 4:7-11

“RAHA YA MILELE UMPE Ee BWANA”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...