DSC_0084
Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias akizungumza na washauri wa Vikundi vya Vijana wasikilizaji juu ya masuala muhimu kuhusiana na kuzuia maambukizi ya VVU na Afya ya Uzazi kwa Vijana wenye umri kati ya miaka 15-24 katika warsha ya kuwajengea uwezo washiriki hao katika matumizi ya mwongozo wa ufuatiliaji wa vipindi kwa wasikilizaji walengwa wa Mradi wa SHUGA Redio inayofanyika kwenye kituo cha Redio Nuru FM mjini Iringa.(Picha zote na Zainul Mzige).

Na Mwandishi wetu

Tafiti zimebaini kwamba Vijana hawatumii Kondomu na hutoa sababu nyingi ikiwa ni pamoja na kutopata ladha wakati wa tendo la ndoa na kwamba inapunguza nguvu na visingizio vingine vingi vinavyopelekea kuashiria hatari ya maambukizi.

Hayo yameelezwa na Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias wakati akizungumza na washauri wa Vikundi vya Vijana wasikilizaji juu ya masuala muhimu kuhusiana na kuzuia maambukizi ya VVU na Afya ya Uzazi kwa Vijana wenye umri kati ya miaka 15-24 katika warsha ya kuwajengea uwezo washiriki hao katika matumizi ya mwongozo wa ufuatiliaji wa vipindi kwa wasikilizaji walengwa wa Mradi wa SHUGA Redio.

“Asilimia 40 ya Wasichana na Asilimia 47 ya Wavulana ndio wenye ufahamu wa kina juu ya maambukizi ya VVU huku asilimia kubwa wakiwa hawana elimu ya kutosha na hawajui afya zao kwa kuwa hawana utamaduni wa kupima VVU ”, amesema Bw. Mathias.
DSC_0184
Mkufunzi wa warsha hiyo Meneja Mawasiliano kutoka Pangani FM, Bw. Abdullah Mfuruki akiwapiga msasa washauri wa Vikundi vya Vijana kwenye warsha ya siku mbili inayoendelea mjini Iringa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...