Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania Jane
Matinde akimkabidhi vifaa vya michezo Mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya soka
ya vijana wa TFF Ayoub Nyenzi kwa ajili
ya mashindano ya Airtel Rising Stars yanayotariwa kuanza kutimua vumbi ngazi ya
mkoa Jumapili ijyayo. Hafla ya makabidhiano ilifanyika jana jijini Dar-es-Salaam.
·
Saidi Meck Sadiki mgeni ramsi ufunguzi Jumapili.
Airtel
Tanzania Jana Alhamis Julai 24, 2014 imekabidhi vifaa vya michezo kwa timu 18 za
wavulana zinazoshiriki michuano ya soka ya vijana wenye umri chini ya miaka 17
maarufu kama Airtel Rising Stars ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi katika
ngazi ya mkoa jijini Dar es Salaam Jumapili 27 Julai 2014.
Dar es
Salaam inajumuisha mikoa ya kisoka ya Ilala, Temeke na Kinondoni. Washiriki
wengine wa mashindano hayo ya kubaini na kuendeleza vipaji watatoka katika
mikoa ya Mwanza, Mbeya na Morogoro. Akizingumza katika hafla hiyo ya kukabidhi vifaa
iliyofanyika kwenye uwanja cha Kumbu Kumbu ya Karume, Mwenyekiti wa kamati ya
vijana ya TFF Ayoub Nyenzi amesema maandalizi yamekamilika.
“Tunatajia kuwa na mashindano yenye ushindani
mkali na ya kusisimua. Napenda kuchukua fursa hii kuwataka viongozi wa soka ngazi
ya mkoa kuhakikisha wanakuwa makini ili kuchagua vijana wenye vipaji kuunda
timu zao za mikoa zitakkazoshiriki fainali za taifa zitakazofanyika jijini Dar
es Salaam mwezi ujao”, alisema Nyenzi.
Mkuu wa
mkoa wa Dar es Salaam Saidi Meck Sadiki anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi
rasmi wa Airtel Rising Stars katika mikoa ya kisoka ya Ilala, Temeke na
Kinondoni utakofanyika kwenye uwanja wa Karume jijini Jumapili ijayo.
Mkoa wa
Mwanza utafungua rasmi michuano yake Agosti 3, ukifuatiwa na Mkoa wa Mbeya
ambao umepangiwa kuanza mashindano yake Agosti 4 wakati mkoa wa Morogoro
utaanza mechi zake Agosti 5. Wakuu wa mikoa husika wanatarajiwa kuwa wageni
rasmi kwenye hafla za ufunguzi wa michuano hiyo.
Mbali na timu za wavulana,
mashindano hayo pia yatashirikisha timu za wasichana katika ngazi ya taifa na
kufanya fainali hizo kuwa na jumla ya timu 12, sita za wasichana na sita za
wavulana. Timu za wasichana zinatoka mikoa ya Ilala, Kinodoni, Temeke, Mbeya,
Mwanza na Zanzibar. Huu ni mwaka wa tatu tangu mashindano ya Airtel Rising
Stars yalipoanza kushirikisha timu za wasichana.
Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania Jane
Matinde amesisitiza nia thabiti ya kampuni ya Airtel ya kuendelea kudhamini
programu hii ya vijana na kulipongeza Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, wizara
inayosimamia michezo na wadau wengine wa soka kwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa
na Airtel kusaidia maendeleo ya soka la vijana.
Michuano wa Airtel Rising Stars ni
mpango kambambe kwa Afrika nzima ambao ni wa kutafuta na kukuza vipaji vya soka
vinavyochipukia kwa wavulana na wasichana wenye umri chini ya miaka kumi na saba
ambao watapata muda wa kuonyesha vipaji vyao na kukutana na wataalamu wa mpira
wa miguu ambao watawapa mafunzo zaidi na kupata nafasi ya kukuza vipaji vyao.
Airtel Rising Stars itahitimishwa
kwa mashindano ya kimataifa ambayo yatashirikisha wachezaji nyota kutoka nchi
22 barani Afrika ambapo kampuni ya mawasiliano ya Airtel inafanya
biashara. Mashindano hayo ya kimataifa
yamepangwa kufanyika nchini Gabon kuanzia Agosti 25 hadi 30.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...