Marehemu Martha Peter Lubuva
24.04.1947 – 18.01.2014

Familia ya Jaji Mstaafu Damian Z. Lubuva inapenda kutoa shukrani za dhati kwa ndugu, jamaa, marafiki na majirani wote ambao wameshirikiana na kutupa misaada ya hali na mali kipindi chote cha kuugua kwake Marehemu Martha Peter Lubuva hadi kifo chake tarehe 18 Januari, 2014 huko India.  Hii ilitupa faraja kubwa katika kipindi hicho kigumu kwa familia.

Kwa namna ya pekee, familia inatoa shukrani kwa Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete, kwa kutuma salaam za rambirambi na Mama Salma kufika nyumbani kutufariji, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Mama Tunu Pinda, kwa kufika kwao kutufariji siku ya mazishi.  Aidha, tunawashukuru Viongozi mbalimbali wa Serikali na Mashirika ya Umma wakiwemo Mh. Benjamini W. Mkapa Rais Mstaafu, Mh. Salim Hamed Salim, Mh. Joseph.S. Warioba na Edward Lowassa, Mawaziri, Mh. Fredrerick Werema, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Majaji.

Mahsusi, Familia inawashukuru sana Baba Askofu wa Jimbo Katoliki Kondoa, Baba Askofu wa Jimbo Katoliki Dodoma na Baba Askofu wa Jimbo Katoliki Mahenge Pamoja na Paroko wa. Parokia ya Mt. Petro Oysterbay kwa kuendesha Ibada ya mazishi kanisani na makaburini.

Kwa namna ya pekee tunawashukuru Viongozi na Watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mahakama, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kanali Kinana, Katibu Mkuu wa CCM, Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii, Wizara ya Afya, Madaktari wa Muhimbili na Hospitali ya Apolo India, Ubalozi wa Tanzania India, Dr. Mvungi, Polisi, Majirani wa Mtaa wa Bongoyo Kaunda na Mazengo, Jumuiya ya Mt. Clara na Kwaya ya Mt. Petro Oysterbay.  Pia tunatoa shukrani kwa Umoja wa Wakazi wa Kondoa Dar – Es – Salaam.

Kwa vile si rahisi kuwataja wote walioshirikiana na familia katika kipindi cha msiba, kwa taarifa hii tunawaomba wote kupokea shukrani zetu za dhati kwa moyo wa upendo mkubwa mlioonyesha kwa familia ya marehemu.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI APUMZIKE KWA AMANI, AMINA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...