Naomba kama kuna mdau mwenye kumbukumbu na mashairi haya aendeleze beti hizi.

1. Karudi baba mmoja toka safari ya mbali
Kavimba yote mapaja na kutetemeka mwili
Watoto wke wakaja ili kumtaka hali
Wakataka na kauli ili iwafae maishani

Akatamka mgonjwa ninaumwa kwelikweli
Hata kama nikichanjwa haitoki homa kali
Roho naona yachinjwa kifo kimenikabili
Kama mwataka kauli semeni niseme nini

Yakawatoka kinywani maneno yenye akili
Baba yetu wa thamani sisi tunataka mali
Urithi tunatamani mali yetu ya halali
Sema iko wapi mali itufae maishani

( ENDELEZENI NAISHIA HAPO)

2. Iddi Amini jasusi joka hili joka kuu
Limefanya uvamizi kuteka ardhi yetu
Hatuna kazi nyingine nikulifunza adabu
Ndipo litakapojua Tanzania ni ya watu

(ANAYEKUMBUKA AENDELEZE)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. 1. KARUDI BABA MMOJA,
    TOKA SAFARI YA MBALI
    KAVIMBA YOTE MAPAJA
    NA KUTETEMEKA MWILI
    WATOTO WAKE WAKAJA
    ILI KUMTAKA HALI
    WAKATAKA NA KAULI
    IWAFAE MAISHANI

    2. AKATAMKA MGONJWA
    NINAUMWA KWELI KWELI
    HATA KAMA NIKICHANJWA
    HAITOKI HOMA KALI
    ROHO NAONA YACHINJWA
    KIFO KIMENIKABILI
    KAMA MWATAKA KAULI
    SEMENI NISEME NINI

    3. YAKAWATOKA KINYWANI
    MANENO YENYE AKILI
    BABA YETU WA THAMANI
    SISI TUNATAKA MALI
    URITHI TUNATAMANI
    MALI YETU YA HALALI
    SEMA IKO WAPI MALI
    ITUFAE MAISHANI

    4. BABA ALIYEKUFANI
    AKAJIBU LILE SWALI
    NINAKUFA MASIKINI
    BABA YENU SINA MALI
    NENO MOJA LISHIKENI
    KAMA MNATAKA MALI
    KAMA MNATAKA MALI
    MTAYAPAYA SHAMBANI
    5. ALIPOKWISHA KUTAJA
    FUMBO HILI LA AKILI
    MAUTI NAYO YAKAJA
    ROHO IKAACHA MWILI
    NA WATOTO KWA UMOJA
    WAKAKUMBUKA KAULI
    KAMA MNATAKA MALI
    MTAYAPATA SHAMBANI

    6. FUMBO WAKATAFAKARI
    WATOTO WALE WAWILI
    WAKAKATA NA SHAURI
    BAADA YA SIKU MBILI
    WOTE WAKAWA TAYARI
    PORI NENE KUKABILI
    KAMA MNATAKA MALI
    MTAYAPATA SHAMBANI

    7. WAKAZIPANDA SHAMBANI
    MBEGU NYINGI MBALIMBALI
    TANGU ZILE ZA MIBUNI
    HATA ZITUPAZO WALI
    NA MVUA IKAJA CHINI
    WAKAONA NA DALILI
    KAMA MNATAKA MALI
    MTAYAPATA SHAMBANI

    8. SHAMBA WAKAPALILIA
    WATOTO WALE WAWILI
    MAVUNO YAKAWAJIA
    WAKAFAIDI UGALI
    WOTE WAKASHANGILIA
    USEMI WAKAKUBALI
    KAMA MNATAKA MALI
    MTAYAPATA SHAMBANI

    9. WAKAWANUNUA NG'OMBE
    MAJIKE KWA MAFAHARI
    WAKAPATA NA VIKOMBE
    MAVAZI NA BAISKELI
    HAWAKUITAKA POMBE
    SABABU POMBE SI MALI
    KAMA MNATAKA MALI
    MTAYAPATA SHAMBANI
    10. WAKAONGEZA MAZAO
    NA NYUMBA ZA MATOFALI
    PALE KWENYE SHAMBA LAO
    WAKAIHUBIRI MALI
    WALIKIWEKA KIBAO
    WAKAANDIKA KAULI
    KAMA MNATAKA MALI
    MTAYAPATA SHAMBANI

    ReplyDelete
  2. Yakamtoka kinywani, baba aliyekufani
    Ninakufa masikini, Baba yenu sina hali
    Neno moja lishikeni kama mnataka mali
    Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

    Alipokwisha kutaja fumbo hilo la halali
    Mauti nayo yakaja,Roho ikaacha mwili
    Na watoto kwa pamoja wakakumbuka kauli
    Kama mnataka mali, Mtayapata shambani.

    ReplyDelete
  3. Muuliza swali (mshairi) leo umeamua kututoa machozi tu sie wa enzi za kipindi kile .....

    Hongera kwa uliyepatia shairi lote la 'Karudi baba mmoja' .... hata mie beti nyingine nilikuwa nimezisahau kabisa.

    Kuhusu shairi la Iddi Amini jasusi ... nadhani wale waliopitia JKT miaka ya 1980 wanaweza kutukumbusha zaidi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...