Msanii Maarufu nchini Tanzania Mpoki a.k.a Muarabu wa Dubai ametua katika Jiji la Frankfurt na kuelekea moja kwa moja katika Jiji la Maraha Aschaffenburg ambapo atalala usiku mmoja na kuendelea na safari siku ya pili  kuelekea  Jiji La Berlin  ambapo atahudhuria mkutano mkuu wa Umoja wa watanzania Ujerumani (U T U), Ngongamano la biashara pamoja na sherehe za muungano wa Tanzania.

Vyanzo vyetu vya habari vinanyetisha kwamba msanii huyo alitua  katika uwanja wa kimataifa  wa Frankfurt mnamo saa 10:30 alasiri na ndege ya shirika la ndege la Ethiopia Airlines akitokea Dar es salaam kupitia Addis Ababa. msanii huyo alipokelewa na mwenyekiti wa watanzania nchini ujerumani.
Tunawatakia watanzania wanaoishi ujerumani kila la heri  na mafanikio katika sherehe hii kubwa na ya aina yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...