Keki Maalum  ambayo imeandaliwa na baadhi ya Wajumbe Wanawake wa Bunge Maalum la Katiba kumpongeza Mjumbe wa Bunge hilo Mh. Asha Bakari Makame kwa umahiri wake wa kupinga udhalilishaji wa kijinsia ndani ya Bunge hilo.
 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mh. Asha Bakari Makame akitoa shukrani zake kwenye hafla fupi ya Kupongezwa kutokana na kutetea jinsia ya Wanawake ndani ya Bunge la Katiba.
  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mh. Asha Bakari Makame akikata Keki Maalum kuashiria uzinduzi wa hafla fupi ya kupongezwa kwake kutokana na msimamo wake ndani ya Bunge Maalum la Katiba linaloendelea Mjini Dodoma.Kushoto yake ni Waziri wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Maendeleo ya Vijana wanawake na Watoto Mh. Zainab Omar Mohammed.
 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mh. Asha Bakari akimlisha Keki Mjumbe mwenzake wa Bunge hilo Mh. Zainab Omar Mohammed kwenye hafla fupi ya kupongezwa kwake.
Mbunge wa Bunge Maalum la Katiba Mh. Waride Bakari Jabu akitoa neno la shukrani kwenye hafla fupi ya Kupongezwa Mjumbe mwenzake Mh. Asha Bakari Makame kwa  msimamo wake ndani ya Bunge hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hivi ndivo pesa za walipa kodi zinavotumika, WALLAHI Mola anawaona na ndio maana mwisho wenu unakuwa mbaya! sipati picha hawa ngulume ameishiaje!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...