Na Swahili Villa Blog

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa


  1. Mwakilishi wetu wa Ugaibuni Bwana Singo amejitahidi sana kueleza maonni ya Viongozi na pamoja na maoni ya Watanzania waishio Ugaibuni. Hotuba yake imeonyesha kwamba wabunge wengi wamepiga makofi na kukubali maombi ya wanadiaspora. Hii ni mara ya kwanza kwa watanzania wanaoishi ugaibuni kuonyesha uzalendo na upendo wa nchi yao-Tanzania. Tuendelee kuchangia kimawazo kwa wabunge ambao wanapinga uraia pacha pamoja na wafuasi wao kwamba watanzania wa ugaubuni na watanzania ni wazalendo popote pale wanakoishi na wako tayari kuimarisha maisha bora ya watanzania wote.

    ReplyDelete
  2. Mdau wa kwanza,

    Watanzania wa Ughaibuni Madiaspora mngekuwa Wazalendo wakweli je, mngekubali kirahisi kupoteza Uraia?

    ReplyDelete
  3. Ongeeni na Prof. Mwesiga Baregu msikie Hoja zake kuhusu kupinga Uraia Pacha!

    ReplyDelete
  4. Asante sana mwana diaspora-Kadari Singo kwa uwakilishi mzuri na sababu nzuri alizozitoa. Watanzania inabidi tubadilike na kuondokana na mawazo mgando. Serikali inabidi iangalie hili swala la uraia pacha kwa vizuri na kuliwekea maanani na kuna watu wao kazi Yao kutukana kwenye comment kuhusu uraia pacha. Mie kuna swala ninataka kulisema, nimefanya kazi kwenye serikali ya Tanznia na pia huku nje nimepata nafasi ya kufanya kazi kwenye serikali. Jamani Watanzania sisi ni wavivu na hatupendi kufanya kazi. Huku nje kila dk na saa unayofanya kazi unairipoti kwenye system, sio kama wanalipwa mshahar mkubwa kama kasumba ya watanzania tuliona mshahara hauna tofauti na watu wanafanya kazi kwa kuiheshimu kazi na ku-deliver na masaa ya kazi ni masaa 8 na dk 15 kwa siku .Mdau wa Sweden

    ReplyDelete
  5. The mdudu,huyu mwakilishi hayo maneno anayasema tu pasipo na uchunguzi nimuulize kwanza hivi huko America hapo Wazanzibar? Jibu ni kwamba wapo tele,mm nipo hapa UK napo wametapakaa kila miji ya hapa na katika Uchunguzi wangu au kwa mujibu wa maneno yao toka midomoni mwao wao ndio Hawautaki hata kuusikia huo muungano sasa ww mwakilishi hivi kweli Ulifanya UCHUNGUZI WA HILO JAMBO? Mpaka useme tuulinde huu muungano sasa swali linakuja kwako na hao wenye mawazo kama yako TUTAULINDA VIPI HUU MUUNGANO ambapo upande mmoja hawautaki? Na kama utaniona mm ni muongo basi uje hapa UK uwaulize mwenyewe kisha usikie jibu watakalokupa,tukija kwenye huu uraia pacha ndugu zangu watanzania tusidanganyane au kujifananisha sisi na mataifa mengine mm hayo mataifa mengine sijui kwajinsi utaratibu wao wa upatikanaji wa PASIPOTI ZAO,ila tukija kwa upande wetu kwajinsi nionavyo mm au hata nyie pia,kwanza kabisa tujiulizeni wenyewe why sisi tulikua tunaingia hapa UK bila ya VIZA na kwa nini waliamua kutuwekea VIZA? Jibu lake hili hapa wahindi wengi wao ndio waliosababisha mpaka tuwekewe VIZA maana pasipoti walikua wanazipata ndivyo sivyo,wanaigeria hivyo hivyo hawa mpaka kesho bado wanazipata ndivyo sivyo,wagana pia so hao wote niliosema hapo Wakisikia Tanzania imepitisha sheria ya uraia pacha hao wote Wataludi huko Tanzania nakujifanya Madiasipora,lazima tuwe makini sana sio tulichukulie kilahisi lahisi tu hili swala la URAIA PACHA.ULINZI WA NCHI KWANZA lasivyo tutakuja kujuta kesho,asanteni sn

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...