Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo mafupi kutoka kwa Afisa Zana za Kilimo wa Wilaya ya Mlele,Lawlence Elias kuhusiana na Mradi wa Mashine ya Kusindika Mpunga mapema leo jioni,katika kijiji cha Mwampuli,Wilaya mpya ya Mlele mkoani Katavi,Mashine hiyo ina uwezo wa kusindika mpunga tani 30 kwa siku.Kushoto ni Mjumbe wa NEC Taifa,Balozi Ali Karume nae akisikiliza kwa makini.Kinana yupo Mkoani Katavi kwa ziara ya siku nne ya kuimarisha uhai wa chama,kukagua na kuhimiza ilani ya Uchaguzi ya 2010.
Mradi wa Mashine ya Kusindika Mpunga kama uonekavyo pichani uliopo katika kijiji cha Mwampuli,Wilaya mpya ya Mlele mkoani Katavi,Mashine hiyo ina uwezo wa kusindika mpunga tani 30 kwa siku.
Katibu Mkuu wa CCM,akikagua Ujenzi wa Mradi wa Maji safi,katika kijiji cha Kibaoni,Wilaya ya Mlele,mkoani Katavi.Tanki hilo la maji safi linatarajia kuhudumia wakazi wa kijiji cha Kibaoni na vijiji vingine tisa.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana wa tatu kulia akishiriki kukusanya mawe pamoja na viongozi mbalimbali wa Taifa,Mkoa na Wilaya (CCM),kukusanya mawe kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa shule ya msingi Maji Moto iliyopo katika kijiji cha Maji Moto,Wilaya mpya ya Mlele mkoani Katavi
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Maji Moto jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara,Nape amewataka wana CCM na wananchi kwa ujumla kuishi kwa amani na upendo katika suala zima la kudumisha amani tulionayo na kuwapuuza wanaotaka kuleta mgawanyiko katika nchi yetu kwa namna moja ama nyingine.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Maji Moto jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara,Kinana ameeleza kuwa kumekuwepo tatizo kubwa kila mahali aendapo kufanya ziara kuhusiana na migogoro ya ardhi kati ya Wakulima na Wafugaji,Wafugaji na Hifadhi ,jambo ambalo linapaswa kufanyiwa kazi kwa umakini mkubwa ,aliongeza kuwa migogoro hiyo imekuwa janga la Taifa,kutokana na idadi ya watu kuongezeka katika maeneo mengi,huku mipaka yake kubaki kama ilivyo kwa muda mrefu.
Kinana akijaribu kuelewesha jambo katika shamba la Ufugaji nyuki la Waziri Mkuu Pinda,katika kijiji cha Kibaoni Wilaya ya Mlele mkoani Katavi mapema leo mchana
Kinana akikatiza kwenye Shamba la Ufuta na Nyuki mara baada ya kujionea ufugaji wa nyuki unavyofanyika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...