Ofisa Polisi Jamii wa Tarafa ya Moipo Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Amiri Mlemba akizungumza jana na wakazi wa Kitongoji cha Sokoni, Kata ya Mirerani, wakati akitoa elimu ya ulinzi shirikishi na polisi jamii.
-----------------------------------------------
ILI kufanikisha dhana ya polisi jamii na ulinzi shirikishi, jamii imetakiwa kuanza kutekeleza suala hilo kwenye ngazi ya kaya, kwani jambo hilo likifanyika kikamilifu, uhalifu utapungua kama siyo kumalizika kabisa hapa nchini.

Wito huo ulitolewa jana na Ofisa Polisi jamii, Tarafa ya Moipo Wilayani Simanjiro, Amiri Mlemba kwenye mikutano ya kuhamasisha polisi jamii na ulinzi shirikishi, iliyofanyika vitongoji vya Songambele na Sokoni, kata ya Mirereni.

Mlemba alisema uhalifu ukizuiwa kuanziwa katika ngazi ya kaya utaweza kumalizika nchini kwani kila familia ikidhibiti uhalifu, Taifa zima litakosa wahalifu na maendeleo yatapatikana.

“Mwenye taarifa ya uhalifu atoe kabla ya tukio la uhalifu kutokea na pia tuna lengo la kuweka picha za watuhumiwa wa uhalifu kwenye kila kata, ili jamii iweze kuwafahamu kwa njia rahisi watuhumiwa wa uhalifu,” alisema Mlemba
Alisema kila mwana jamii akijihisi kuwa uhalifu una mwathiri yeye binafsi na akiuchukia uhalifu kwa moyo mmoja, matukio ya uhalifu yatamalizika kama siyo kupungua katika maeneo wanayoishi.

“Kazi ya kukamata mhalifu siyo ya polisi peke yake, kwani hapa Mirerani kuna zaidi ya watu 40,000 na tupo askari polisi 51 hivyo kila kwenye kila ubalozi pawepo na polisi jamii ili kudhibiti uhalifu,” alisema Mlemba.  

Hata hivyo, Ofisa Mtendaji wa kata ya Mirerani, Steven Wanga alisema polisi jamii huwa wanatoa huduma hiyo wakishirikiana na polisi kata, hata sehemu ambazo hazina vituo vya polisi katika maeneo tofauti hapa nchini.
“Kwenye maeneo niliyowahi kufanya kazi kama katika kata za Terrat na Ngorika, tulikuwa tunawatumia polisi jamii kukomesha uhalifu na polisi kata wanafungua kesi na tunawashtaki wahalifu,” alisema Wanga. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...