Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendela kushoto, akimkabidhi  kikombe Mkurugenzi wa Wateja Binafsi na wa kati wa Benki ya CRDB, Nelia Ndosa wakati wa kutoa tuzo zilizotolewa na ULUGURU. Benki hiyo imepata tuzo ya heshima ya Uluguru kutokana na mchango mkubwa uliotolewa na benki hiyo katika kuisaidia jamii ya watu wa Mkoa wa Morogoro. 
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi na wa Kati wa Benki ya CRDB, Nelia Ndosa kushoto na Mkurugenzi wa benki hiyo Mkoa wa Morogoro Pendo Issey katikati wakiwa wameshikilia kombe walilokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa huo, Joel Bendera hayupo pichani wakati wa utoaji wa tuzo za Heshima za ULUGURU kulia ni mfanyakazi wa benki hiyo.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB Mkoa wa Morogoro wakiwa wameshikilia kombe walilokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa huo wakati wa kupokea zawadi  za Heshima  zilizotolewa na ULUGURU AWARD.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na  wafanyakazi wa Benki ya CRDB pamoja na kombe lao. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...