Embassy pics 016Mh.Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico Liberata Mula mula akizungumzia maandalizi ya sherehe za miaka 50 ya muungano ofisini kwake Washington Dc Jumatano, Aprili 23, 2014. Embassy pics 037Mwenyekiti mwenza wa kamati ya maandalizi afisa ubalozi Suleiman Saleh akijibu maswali ya mabloger wa DMV,kulia kwake ni Dickson Mkama wa Swahili TV blog. Embassy pics 018Mh, balozi akijibu maswali kushoto ni Sunday Shomari na kulia kwa balozi ni Mubelwa Bandio wa Kwanza production. Embassy pics 007Mh.balozi akishauriana jambo na mkuu wa kitengo cha mawasiliano katika wizara ya mambo ya nje Bi.Mindi Kasiga ambaye atakuwa ndio MC wa shughuli hiyo. 

 Katika mkutano huo na mablogger wa DMV Mh,Balozi Liberata Mula mula amesema maandalizi sasa yamepamba moto ikiwa ndio count down kuelekea D-day (wakihesabu siku zilizobaki kuelekea siku ya kilele cha maadhimisho hayo ya miaka 50 ya muungano wa Tanzania). 

 Mh.balozi ameasa watanzania wa DMV na majimbo ya karibu kujitokeza kwa wingi katika siku hiyo kwani ni siku ya kihistoria kwa taifa la Tanzania na inafanyika kwa mara ya kwanza Washington Dc. Ameeleza kuwa kila kitu kitu kiko tayari na katika siku hiyo ameeleza mtiriririko mzima ambapo sherehe zitaanza asubuhi katika ofisi za ubalozi wa Tanzania Dc ambapo kutakuwa na "Open house " ikiwa na maana maonyesho ya kuitangaza Tanzania ilikotoka, iliko na inakoelekea ikiwa ni pamoja na maonyesho ya mitindo , utalii na mavazi ya mtanzania , shughuli hiyo itaanza saa 4 asubuhi mpaka saa tisa alasiri.

 Na katika hafla hiyo kutakuwa na vyakula vya aina mbali mbali vya Tanzania kuanzia kifungua kinywa mpaka chakula cha mchana ambapo kutakuwa na vyakula mbali mbali vya Tanzania kama vile mihogo, maandazi, kalmati n.k. vitafunwa hivyo vipo zaidi ya aina 22, aidha amesema pia kutakuwa na chakula cha mchana ikiwa utakosa cha asubuhi kama vile pilau, maharage, mihogo ya Nazi n.k. Mchana chakula kitapatikana kati ya saa 7 hadi 8 alasiri pia kutakuwa na vinywaji kutoka Tanzania kama vile Konyagi, bia za Tanzania, Juice na wine ambavyo tayari vimeshawasili. 

Vyakula hivi ni bila malipo yeyote amesisitiza. Kutakuwa na maonyesho mbali mbali ikiwa ni pamoja na mavazi, mitindo na michezo ya kuigiza.Na baada ya hapo jioni kuanzia saa mbili usiku kutakuwa na hafla rasmi ya usiku "Tanzania Muungano Night" ambapo wote mnaalikwa bila kukosa na bila kuchelewa katika ukumbi wa Matnice Events and Conference Center 7925 Central Avenue Capital Heights Md 20743. 

 Wageni rasmi ni kutoka pande mbili za muungano ambao Mh. Mwigulu Nchemba (Mbunge na naibu waziri wa fedha na Uchumi Tanzania bara na upande wa Zanzibar atakuwepo Mh. Dr.Mwinyihaji Makame mwakilishi na waziri wa nchi ofisi ya rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Zanzibar na watawasili kuanzia Ijumaa hapa Washington Dc. 

Wageni kutoka serikali ya Marekani ni balozi Donald Tate Boum naibu waziri wa mambo ya nje anayeshughulikia masuala ya Afrika pamoja na viongozi wa biashara na viongozi wa mabalozi kutoka kila kanda. Shughuli ya usiku itaanza saa mbili kamili mpaka Liamba ambayo kutakuwa na vyakula vya kila aina kwa ajili yako hakuna kiingilio wala malipo ya chakula ila katika upande wa vinywaji ni mfuko wako tu kunywa unachotaka alisisitiza balozi. 

 Kutakuwa na waigizaji, waimbaji , ngonjera , muziki na kila aina ya burudani na siku ya Jumapili itakamilishwa na kabumbu "Muungano soccer tournament" kuanzia saa tisa alasiri huko Fairland recreational Park 3928 Green castle Rd, Fairland Md 20866.

 Timu ya Zanzibar Heroes ya DMV ambayo itapambana na Kilimanjaro stars ya DMV na balozi atafungua mechi hiyo kwa kupiga mpira na ameahidi atafunga goli , aidha Mh.balozi amesema michezo ni mingi ikiwa ni pamoja na kuvuta kambi n.k na kuwaomba wakazi wa DMV na familia zao wajitokeze kwa wingi. Washindi watapata medali na vikombe aliongeza balozi akisema "hamtatoka mikono mitupu na nyama choma ni za kutosha sana zitakuwepo zikiongozwa na wanajumuiya wa DMV wenyewe".

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...